Mastar wawili tajika wabongo wapatwa na Coronavirus
Leo imekuwa siku ya huzuni nchini Tanzania baada ya wawili hawa kutangaza kuwa na virusi vya Corona.
Wawili hawa ni msanii tajika mwanaFA na meneja mkuu wa diamond platnumz bwana sallam SK. Katika maongezi yake hapo awali, mwanaFA amewahimiza wa Tanzania kutahadhari sana na ugonjwa huu akiwahimiza wanainchi kutumia mapendekezo yanayotolewa na vituo vya afya.
mwanaFA amesema kwa Sasa amejitenga ili kupokea matibabu na familia yake iko salama kwani kutoka atoke Safari, hajakutana na watoto wake. Ameongeza kuwa mashabiki wake wasiwe na wasiwasi kwani hii ni homa tu na baada ya mda mfupi atakuwa sawa
Tunawaombea wawili hawa nafuu ya haraka na bilashaka mwenyezi mungu atawaponya na wataendelea na ujenzi wa taifa
418 total views, 1 views today
Aky msiwe na wasiwasi mungu yupo, hakuna lolote linalo mshinda mungu, ntazidi kuwaombea ndugu zangu wa tanzania,
Ndugu zangu, mungu yupo, hakuna linalo mshinda, kumbuka aliwapo viwete, vipofu, akafufua wafu, sembuse corana, hio sio kitu kwake mungu, atakuponya na itakua n ushuhuda,